Hali nchini Pakistan | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 28.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Hali nchini Pakistan

Mafuriko yatishia maisha katika maeneo ya kusini,mwezi mmoja baada ya janga baya kabisa la mafuriko kuwahi kuisibu Pakistan

Kambi za wahanga wa mafuriko nchini Pakistan

Kambi za wahanga wa mafuriko nchini Pakistan

Mwezi mmoja tangu mafuriko mabaya kabisa kulisibu eneo la kaskazini la Pakistan,malaki ya watu wameanza kuyapa kisogo maskani yao hii leo baada ya mto Indus kufurika na kuvunja mabwawa zaidi katika maeneo ya kusini ya nchi hiyo. Muakilishi wa serikali ya jimbo la Sindh anasema watu zaidi ya milioni mbili na laki mbili hawana mahala pa kuishi katika maeneo yanayopakana na mji wa Thatta.Wakaazi laki tatu wa mji huo wameshahamishwa.

Tangu mapema mwezi wa Agosti,watu milioni sabaa wameyapa kisogo maskani yao katika eneo la Sind-milioni moja kati yao katika kipindi cha siku mbili zilizopita"-amesema hayo Gulam Ali Pasha,alipohojiwa na shirika la habari la Ufaransa AFP.

Wakati huo huo mafuriko yameanza kukupwa katika maeneo ya kaskazini na kati ya Pakistan.

Watu zaidi ya milioni nane wanakumbwa na maafa ya mafuriko na karibu milioni tano waliovunjikiwa na maskani yao wanahitaji misaada ya dharura.

Jeshi la shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Bundeswehr limetuma ndege iliyosheheni majenereta matatu ya umeme na tani 18 za vyakula vya watoto wachanga kuwasaidia wahanga wa mafuriko nchini Pakistan.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir

Imepitiwa na:Mohammed Dahman

 • Tarehe 28.08.2010
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OyNc
 • Tarehe 28.08.2010
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OyNc
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com