1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali inatatanisha nchini Guine

Oumilkher Hamidou23 Desemba 2008

Spika wa bunge anasema sio wanajeshi wote walioko nyuma ya kepteni Davis Camara

https://p.dw.com/p/GM2P
Majeruhi wa maandamano dhidi ya Lansana ContePicha: AP



Baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika litakutana kwa kikao cha dharura leo au kesho kuzungumzia hali ya mambo nchini Guinee baada ya kufariki dunia rais Lansana Conte na uvumi wa njama ya mapinduzi nchini humo.


"Ikiwa njama ya mapinduzi itathibitika,basi hali hiyo itakua ni sawa na kuiendeya kinyume katika na muongozo wa kisheria wa Afrika unaopiuga marufuku moja kwa moja kubadilishwa serikali kinyume na katiba."Hayo ni kwa mujibu wa kamishna wa Umoja wa Afrika anaeshughulikia masuala ya amani na usalama,Ramtane Lamamra.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Umoja wa Afrika Jean Ping ataitumia hoja hiyo,kama ilivyotajwa katika azimio la Lome linalopiga marufuku mapinduzi,ili kuitisha mkutano wa dharura wa baraza la amani na usalama-amesisitiza bwana Lamaamra,akiwa katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Abeba.Amezungumzia uwezekano wa kuzuwiliwa Guine kushiriki katika mikutano na harakati nyenginezo za Umoja wa Afrika.


Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa afrika Jean Ping,amemtumia risala spika wa bunge la Guine,Aboubacar Sompare ambae kikatiba ndie anaestahiki kushika nafasi ya rais hadi uchaguzi huru utakapoitishwa.Wananchi wa Guine wao wanasema

"Wananchi wanataraji kumuona spika wa bunge akiongoza kipindi cha mpito,kuandaa na kuzitisha uchaguzi mkuu haraka,uchaguzi utakaokua huru na wa uwazi na kwamba mshindi anatambuliwa na vyama vyote vya kisiasa."


Hali inatatanisha nchini Guine baada ya kepteni Moussa David Camara kutangaza redioni kwamba serikali na taasisi zote zimevunjwa na katiba kusitishwa.


Wanamapinduzi hao wanaosema wameunda "baraza la taifa kwaajili ya demokrasia na maendeleo (CNDD) wamewataka "mawaziri na maafisa wote wa serikali na maafisa wakuu wa kijeshi wakusanyike katika kambi kuu ya kijeshi ya nchi hiyo ,kwa kile walichokiita "kudhamini usalama wao."


Spika wa bunge Aboubacar Sompare amesema hafikiri kama jeshi lote linamuunga mkono kepten Moussa David Camara.


"Ni njama ya mapinduzi ,lakini siamini kama wanajeshi wote wanaiunga mkono" amesema spika huyo wa bunge alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Ufaransa France 24.Anaamini anasema wengi wa wanajeshi wanaiunga mkono serikali.


Mjini Conacry,maripota wanazungumzia juu ya dazeni kadhaa za vikosi vya wanajeshi wakisaidiwa na vifaru wanaoelekea katika kasri la rais na jengo la benki kuu.


Umoja wa ulaya umetoa mwito katiba iheshimiwe nchini Guine.Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ufaransa, imesema viongozi halali wa Guine ndio wanaodhibiti hali ya mambo.


Pata shika hii imezuka mara baada ya tangazo la kufariki dunia rais Lansana Conte,jana usiku, baada ya kuitawala kwa mkono wa chuma nchi hiyo kwa muda wa miaka 24.