Hali ikoje Iran na Netanyahu na la dola la wsapalestina | Magazetini | DW | 16.06.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Hali ikoje Iran na Netanyahu na la dola la wsapalestina

Ni mada 2 kuu zilizochambuliwa leo na wahariri:

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani, yameichambua Iran baada ya ya uchaguzi; waziri mkuu Netanyahu wa Israel na masharti yake ya amani na wapalestina.

Gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND juu ya hali nchini Iran.Laandika:

"Fimbo ya nchi za ulaya ya kuadhibu utawala wa Iran ina mpaka wake.Mtu kama rais Ahammadinejad anafurahia sifa ya kutoheshimiwa,hatamtumilia vitisho vya vikwazo vya kisiasa.Mbaya ni kumuona msemaji wa sera za nje wa Umoja wa ulaya Bw.Javier Solana na nchi fulani za Umoja wa Ulaya, kudai hivi sasa mazungumzo na Iran yasivunjwe na kwa kudai hivyo kuwapa Mamullah uwanja wa kufanya watakavyo.

Umoja wa Ulaya utakiuka misingi ya desturi zake endapo zitakabili kutumiliwa nguvu na mkomoto wapinzani wa utawala kana kwamba hakujatokea kitu nchini Iran.Kwani, ni katika kutetea maadili ya desturi hizo hizo ndipo waandamanaji mjini Teheran wamekulamkomoto na kutiwa nguvuni."

Likiendeleza mada hii,gazeti la WESTDEUTSCHE ZEITUNG laandika kwa jicho la sera za kilimwengu,mwishoe, uamuzi hautakatwa mjini Teheran iwapo wafuasi wakakamavu watashinda au la, bali mjini Washington,Marekani.Itamtegemea Rais Obama atakavyoamua:Gazeti laongeza:

"Wanaopepea moto na nchini Israel si wachache, wana hamu kuona hayafanyiki mazungumzo kati ya Iran na Marekani.Wangependa leo kabla ya kesho kuichukulia Iran hatua kali kijeshi na hata kutojali iwapo kwa kutenda hivyo kutautosa ulimwengu msibani.Hii yapasa kuzuwiliwa isitokee ."

Likitukamilishia mada hii ya Iran, gazeti la MAIN-POST linasema hali ya mambo nchini Iran ni ya kutatanisha na hata kwa wanadiplomasia wa eneo hilo.Kutoka Washington hadi Berlin mtu anajikuna kichwa tangu miaka mingi sasa,nani anaamua nini nchini Iran.Gazeti laongeza:

"Sasa inatatanisha hata zaidi kupata wa kuzungumza nae anaetegemeka katika ule mchezo wa kamari juu ya hatima ya mradi wa nuklia wa Iran.

Matumaini ya kuanza enzi mpya katika usuhuba kati ya marekani na Iran,sasa yamefifia."

Gazeti la Nuremberger Zeitung linachambua masharti ya kufunga amani na wapalestina alioyatoa juzi waziri-mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu:

gazeti linahisi kuwa Netanyahu anapitisha tu wakati .Anahisi mbinyo kutoka Washington na wakati huo huo hali ya kufadhahisha nchini Iran ambayo inajitanua katika eneo zima. Gazeti lasema zaidi:

"Kuzidi kupata nguvu na kuimarika kwa jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo hautapita muda yaweza kuwa dola la kinuklia,kutaangaliwa tangu nchini saudi Arabia,Misri,Uturuki na hata Urusi kuwa ni kitisho cha kuharibu utulivu katika eneo hilo.

Nuremberger Zeitung laongeza:

"Israel kinyume chake, licha ya ila zote zilizotolewa kwake kwa jinsi ilivyopambana na wapalestina,imejitokeza ni nguzo ya utulivu katika eneo hilo-nguzo ambayo haifai mtu kuidhofisha."

LAUSITZER RUNDSCHAU linatumalizia kwa maoni haya juu ya Netanyahu:

"Ilidhihirika dhahiri-shahiri tangu mwanzo kuwa Netanyahu hangeweza kuthubutu kusema anabisha kabisa kuundwa kwa dola la wapalestina ikiwa haingetaka mpambano wa uso kwa uso na Marekani-mpambano ambao ungemalizikia kuanguka kwake Netanyahu.

Lakini kwa upande mwengine,amelazimika kuzingatia na kutia maanani upinzani mkali wa walowezi wa kiyahudi na wazalendo serikalini mwake wanaozima juhudi za kuleta suluhisho la dola mbili na ndio maana amezunguka upande mwengine kutotumia lugha alioitumia Rais Obama ya kuridhia moja kwa moja dola 2."

Muandishi: Ramadhan Ali/DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman