1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GM Opel Magna

Sekione Kitojo11 Septemba 2009

Kampuni ya kuunda magari ya Opel baada ya miezi kadha ya mivutano hatimaye itauzwa kwa kampuni ya kutengeneza vipuri vya magari ya Magna.

https://p.dw.com/p/JcvT
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, kushoto, akizungumza na waziri wa fedha Peer Steinbrueck tarehe 2. April 2009.Picha: AP

Kampuni ya kuunda magari ya Opel baada ya miezi kadha ya mvutano hatimaye itauzwa kwa kampuni ya kutengeneza vipuri vya magari ya Magna. Kampuni mama ya General Motors imetangaza jana Alhamis kuuza asilimia 55 ya hisa za Opel kwa kampuni hilo mali ya Austria na Canada pamoja na mshirika wake benki ya Sberbank ya Urusi. GM tawi la Ulaya limeeleza jana , kwa mujibu wa mapendekezo muhimu ya bodi ya ushauri ya General Motors. Asilimia kumi nyingine zitachukuliwa na wafanyakazi. GM kwa hiyo itabakiwa na asilimia 35 ya hisa katika kampuni hiyo mpya itakayojulikana kama New Opel. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anasema kuwa kuna uwezekano sasa wa Opel kuanza upya. Je ni siku nzuri kwa Opel? anauliza Henrik Böhme.

Mshindi ni Magna. Ilikuwa ni shangwe kubwa katika mji wa Rüsselsheim, huko Bochum pamoja na miji mingine ambako Opel ina karakana zake wakati taarifa za kwanza zilipojitokeza. Magna ulikuwa ni uamuzi mkubwa, kwasababu Magna ilikuwa ndio kampuni waliyoipendelea. Ghafla kampuni hiyo imejitoa kutoka mikononi mwa Wamarekani , ambapo kwa miaka kadha Opel imenyonywa , kwa muda wa miongo miwili iliendeshwa vibaya, na faida ya ubora wa magari hayo hauridhishi.

Uhusiano wa kimapenzi ni haukuwapo tena kwa muda mrefu sasa, katika ndoa hii iliyofungwa kiasi miongo nane iliyopita. Hivi sasa kampuni mama ya General Motors mjini Detroit baada ya mvutano wa hapa na pale imeamua, mwanae huyo kumuachia atoke nyumbani. Kampuni hiyo hata hivyo haipaswi kulipa sehemu ya mahari, malipo hayo yatabebwa na walipa kodi wa Ujerumani . Euro bilioni 1.5 za deni la kuiendesha kampuni hiyo zimekwisha tolewa tayari na serikali mjini Berlin, ama sivyo Opel hii leo isingekuwapo. Na kwa hiyo pamoja na kununuliwa huko, serikali ya Ujerumani itatoa kiasi cha Euro bilioni 4.5 kwa ajili ya mtaji wa kuanzia kwa kampuni ya Magna hapo baadaye.

Pamoja na hayo fedha hizo ndio GM ilihitaji kwa ajili ya kuiokoa Opel. Iwapo GM ingeweza kuendelea kuimiliki Opel , huenda baada ya taarifa ya ukaguzi wa mahesabu wa kampuni ya KPMG ingedai kiasi kingine cha dola bilioni 6 za dharura , ili kuweza kulipia madeni ya nyuma, kwa wizara ya fedha ya Ujerumani. Hata hivyo fedha hizo General Motors haina. Mwanguko ni mkubwa , lakini pia mwanzoni mwa mwaka huu kampuni hilo kubwa kabisa la uundaji magari duniani kwa haraka liliendesha hatua ya muflisi, lakini hii ndio sababu , kampuni hiyo inaweza kutupa deni lake kubwa kwa serikali.

Serikali ya Marekani kwa sasa inatoa usaidizi wa dola bilioni 50 kwa mgonjwa wake huyu mashuhuri. Mvutano huu kuhusu Opel umeanza kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa Ujerumani. Kansela wa Ujerumani Merkel kutoka chama cha CDU pamoja na mgombea kiti cha ukansela Frank - Walter Steinmeier wa chama cha SPD waliamua mapema kuwa kampuni ya Magna ndio muwekezaji anayependelewa.

Mkakati ambao unaweza pia kwenda kombo. Wakianza hivi sasa kushangilia kuwa wameweza kuiokoa Opel , huenda wote wawili wakaabika. Kuingilia kwa kiasi kikubwa kwa serikali katika uamuzi wa kibiashara, ni hali mbaya , hususan kutokana na msingi wa kutoa mabilioni mengi ya Euro kwa ajili ya uokozi kutoka serikalini.

Mwandishi Böhme, Henrik / ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri: M.Abdul-Rahman

E N D E