Hakuna kugawana mali nusu kwa nusu baada ya talaka | Matukio ya Afrika | DW | 15.05.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Hakuna kugawana mali nusu kwa nusu baada ya talaka

Mahakama kuu nchini Kenya imekataa ombi la kubadilishwa kwa sheria ili kuruhusu wanandoa kugawana mali yao nusu kwa nusu wakati wa talaka.

Mahakama kuu nchini Kenya imekataa ombi la kubadilishwa kwa sheria ili kuruhusu wanandoa kugawana mali yao nusu kwa nusu wakati wa talaka. Wanaharakati wamesema uamuzi huo ni pigo kwa haki za wanawake nchini humo. Chama cha wanawake mawakili wa Kenya FIDA ambacho pia kinatetea haki za wanawake kiliwasilisha ombi mahakamani mwaka 2016, kikisema kuwa kipengee cha mali ya wanandoa ni kinyume na sheria kwa kuwa kilimpa mwanandoa umiliki wa mali tu ambayo alileta. Chama hicho kilisema kuwa katiba ya Kenya inasema wanandoa wana haki sawa hivyo kipengee hicho kinawaathiri wanawake ambao wanaweza kupatwa na hasara ya fedha wakati ndoa inapovunjika. Katika uamuzi wake, mahakama hiyo ilisema kubadilisha sheria hiyo kutafungua mlango kwa mtu kuingia katika ndoa na apate mali nyingi kuliko anayostahili kupata wakati wa talaka

 

 

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com