Hakuna Ebola Tanzania | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Hakuna Ebola Tanzania

Serikali ya Tanzania leo imekanusha uvumi wa kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola nchini humo lakini imewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya tishio la ugonjwa huo unaosambaa kwa kasi katika nchi za Afrika Magharibi

Vipimo vimeonyesha kuwa waliokuwa wameshukiwa kuugua Ebola wanao ugonjwa wa kawaida

Vipimo vimeonyesha kuwa waliokuwa wameshukiwa kuugua Ebola wanao ugonjwa wa kawaida

Hatua hiyo inakuja baada ya kuwepo ripoti kwamba watu wawili mmoja raia kutoka Benin waliwasili jana nchini na baadaye kugundulika kuwa na dalili zote za ugonjwa huo ambao tayari umepoteza maisha ya maelfu ya watu katika nchi za Liberia, Siera Leone na Nigeria.

Kutoka na taarifa hizo kilijitokeza kwa hali ya taharuki kutoka kw amakundi mbalimbali ya watu walioingiwa na hofu kutokana na ukweli kwamba ugonjwa huo hadi sasa bado hauna tiba wala chanjo.

Lakini akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwali Julius Nyerere Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaaban Mwijaka alitupilia mbali taarifa hizo akisema kuwa hadi dakika hii Tanzania haijapata mgonjwa yoyote wa Ebola.

Amesema Hakuna mgonjwa yeyote wa Ebola na kusisitiza kuwa waliokuwa wakishukiwa walikuwa na magonjwa ya kawaida. Datari Mwijaka amesema mikakati imefanywa kuhakikisha kwamba watu wote wanaowasili kutoka maeneo yenye ugonjwa huo wanakaguliwa ipasavyo.

Mikakati ya Ukaguzi

Miongoni mwa mikakati iliyowekwa ni kuweka vituo vya kuwatenga wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola

Miongoni mwa mikakati iliyowekwa ni kuweka vituo vya kuwatenga wanaoshukiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola

Katika hatua nyingine serikali imetangaza mikakati yake ya kukabiliana na kitisho cha ugonjwa huo ikiwamo kuendesha ukaguzi wa mara kwa mara kwa wasafiri wanaoingia kupitia maeneo ya mipakani.

Pia imeongeza maofisa wake kwenye viwanja vya ndege huku ikizimulika kwa karibu ndege zinazofanya safari katika maeneo ya Afrika Magharibi ambako ndiko kwenye idadi kubwa ya wagonjwa hao. Wasafiri wanaoingia kwa ndege za Kenya Airways na Rwandair ambayo hufanya safari kwenda Afrika Magharibi, watakuwa wakifanyiwa vipimo katika juhudi za kuhakikisha wahaingizi vi´rusi vya Ebola nchini Tanzania.

Vifaa maalum kusambazwa

Pamoja na mikakati hiyo serikali imesema kuwa kuanzia wiki ijayo itasambaza vifaa maalumu katika viwanja vyake vyote vya ndege katika kile kinachoelezwa kwamba kukabiliana na tishio la ugonjwa huo.

Wakati hayo yakiendelea Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limeonya juu ya uwezekano wa kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo iwapo kutakosekana juhudi za pamoja kutoka mataifa yaliyoendelea na yale ya Afrika

Mlipuko wa ugonjwa huo ambao kwa mara ya kwanza uligundulika mwaka 1976 tayari umepoteza maisha ya raia zaidi ya 1000 huku visa vya ugonjwa huo vikizidi kuongezeka

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com