Hakielimu yakosoa matokeo ya ya kidato cha 4 | Masuala ya Jamii | DW | 28.01.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Hakielimu yakosoa matokeo ya ya kidato cha 4

Shirika lisilo la kiserikali la haki elimu nchini Tanzania limesema kuwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne sio ya kujivunia kutokana na zaidi ya nusu ya watahiniwa kupata ufaulu wa daraja la nne na daraja sifuri.

Matokeo yaliyotoka juma lililopita na kutangazwa na baraza la mitihani nchini, NECTA yanaonesha ufaulu umeongezeka kwa asilimia moja nukta mbili tisa huku takriban asilimia sitini na nane wakipata ufaulu wa daraja la nne na sifuri na waliopata ufaulu wa daraja la kwanza hadi ya tatu ikiwa takriban asilimia 32.

John Kalage mkurugenzi mtendaji shirika la Hakielimu ameiambia DW kuwa matokeo hayo yanaakisi uhalisia wa elimu nchini na changamoto zake ambazo zinahitaji kwa kiwango kikubwa kuangaliwa kwa jicho la kipee na kuongeza kusema kuwa.

Amesema katika ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2016 ambayo ilitathmini juu ya utolewaji wa huduma ya elimu na afya, ambapo walimu kadhaa wa masomo ya hisabati walipewa mtihani na asilimia themanini walipata chini ya asilimia themanini huku waliobaki wakipata juu ya hapo.

Katika matokeo hayo pia yanaonesha ufaulu katika masomo ya sayansi watahiniwa hawakufanya vizuri, jambo ambalo linatafsiriwa kuwa lazima jitihada zianzie kwa walimu.

Kalage amesema shule za binafsi kwa mara nyingine tena zinaonekana kufanya vizuri katika matokeo hayo ambazo inakadiriwa inachukua asilimia sita pekee ya wanafunzi huku asilimia tisini na nne wakibaki katika shule za umma ambazo zimeonesha jicho la ziada linahitajika ili kupandisha kiwango cha ufaulu katika shule hizo zinazochukua kiwango kikubwa zaidi cha wanafunzi nchini.

Mwandishi: Hawa Bihoga Dw Dar es Salaam

Mhariri: Grace Patricia Kabogo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com