Haki za wenyeji asilia Australia | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Haki za wenyeji asilia Australia

Waziri Mkuu wa Australia Kevin Rudd amewaomba radhi wenyeji wa Australia-Aborigines kwa maonevu yaliyowafika watu hao kwa muda wa miaka mingi

default

Waaborigines wakisheherekea nje ya bunge baada ya waziri mkuu kuomba radhi.

Hatua ya waziri mkuu huyo imefungua ukurasa mpya katika uhusiano baina ya wanyeji hao na serikali ya Australia.


Akizungumza bungeni,kuwaomba radhi rasmi wenyeji asilia wa Australia, waziri Mkuu Rudd amesema mjini Canberra kuwa sheria na sera za nchi zilisababisha, uchungu na maonevu kwa watu hao ,kwa muda wa miaka mingi.

Amesema samahani kwa watu hao ,kwa mateso na dhulma iliyowafika.

Waziri Mkuu Rudd amesema wakati sasa umefika wa kufungua ukarasa mpya katika historia ya Australia kwa kusahihisa makosa waliyofanyiwa wenyyeji wa nchi hiyo, ili kuweza kusonga mbele kwa nia safi.

Katika hotuba yake waziri mkuu huyo pia aliomba samahani kwa niaba ya mabunge na serikali zilizopita nchini Australia kwa kutekeleza sera zilizosababisha maonevu makubwa kwa wakazi asilia wa nchi hiyo. • Tarehe 13.02.2008
 • Mwandishi Abdu Mtulya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D75t
 • Tarehe 13.02.2008
 • Mwandishi Abdu Mtulya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D75t
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com