Haki za watoto barani Afrika - Vijana wenye uwezo | Noa Bongo | DW | 10.05.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

Haki za watoto barani Afrika - Vijana wenye uwezo

Watoto wa Afrika mara nyingi wanapitia maisha magumu. Noa Bongo inajaribu kuangazia changamoto hizi na haki za kimsingi za watoto barani Afrika.

Maisha si matamu kama kipande cha keki kwa watoto wengi barani Afrika

Maisha si matamu kama kipande cha keki kwa watoto wengi barani Afrika

Huku watoto wengi wa Kizungu wanapokuwa wakicheza na Wanasesere, wenzao kutoka barani Afrika wanalazimika kufanya kazi wakiwa wadogo sana. Katika mataifa mengi barani humu, watoto huenda shule wakati wa asubuhi na kisha kuwasaidia wazazi wao na kazi za shambani wakati wa alasiri. Isitoshe wengi wao hulazimika kuanza maisha ya kujitegemea wakiwa na umri mdogo sana kwa sababu wazazi wao wameshindwa kuwatunza.

Watoto barani humu wanapitia maisha magumu. Na wanakumbwa na tisho la kufariki wakiwa na umri mdogo sana. Tisho la vifo miongoni mwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ni kubwa zaidi barani Afrika kuliko mabara mengine. Baadhi yao wanaishi katika sehemu zinazokumbwa na mizozo na ukosefu wa usalama. Mbali na hayo si rahisi kupata elimu bora ikilinganishwa na wenzao kutoka mabara ya Asia, Marekani na Ulaya.

Noa Bongo inaangazia hadithi ya kuhuzunisha kuhusu masaibu ya Watoto barani Afrika. Yote haya ni kutokana na juhudi zao wenyewe, na pia za watu wanaotetea haki za watoto katika juhudi za kubadilisha maisha yao. Pia tunaangazia ufanisi uliopatikana, kwa mfano kuanzishwa kwa bunge la watoto linalotetea haki za watoto nchini Nigeria.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako; vinasikika katika lugha sita: Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Hausa, Kireno na Amharik. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni nchini Ujerumani.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com