Haki za binadamu zinahitaji kushughulikiwa kwa ujasiri, yasema ripoti ya Human Rights Watch. | Matukio ya Kisiasa | DW | 15.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Haki za binadamu zinahitaji kushughulikiwa kwa ujasiri, yasema ripoti ya Human Rights Watch.

Ripoti ya Human Rights Watch imemlaumu rais Bush wa Marekani pamoja na kutoa wito kwa rais mteule Barack Obama.

Rais mteule Barack Obama akiwa na rais George W. Bush wakizungumza katika ofisi ya rais mjini Washington . Rais Bush amelaumiwa katika ripoti ya Human Rights Watch kutokana na kukiuka haki za binadamu katika mapambano dhidi ya ugaidi

Rais mteule Barack Obama akiwa na rais George W. Bush wakizungumza katika ofisi ya rais mjini Washington . Rais Bush amelaumiwa katika ripoti ya Human Rights Watch kutokana na kukiuka haki za binadamu katika mapambano dhidi ya ugaidi

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch jana limetoa ripoti yake ya mwaka mjini Washington. Ripoti hiyo imemshambulia rais George Bush wa Marekani na kutoa wito kwa rais mteule Barack Obama. Mataifa kadhaa ya Afrika yametakiwa kufanya juhudi za kutekeleza haki za binadamu. Afrika kusini, Urusi, China na India nazo zimekosolewa.

Ripoti hiyo inayohusu hali ya haki za binadamu duniani , kutoka kwa shirika binafsi lenye ushawishi mkubwa la Human Rights Watch imekuja wakati muafaka. Wakati katika ukanda wa Gaza mamia ya raia wanauwawa kutokana na mashambulio ya kijeshi ya Israel, inamtayarisha mrithi wa rais Bush mjini Washington , na kutoa matumaini makubwa kwa dunia, na pia katika msingi wa utekelezaji wa haki za binadamu.


Kutokana na rais Bush kupinga sheria za haki za binadamu katika vita vyake dhidi ya ugaidi, mtu anaweza pia kusema amejiweka katika nafasi ngumu. Barack Obama , rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika , anaingia madarakani na kubeba matumaini ya wengi, kwamba Marekani kwa mara nyingine tena itahakikisha kuwa ni mtetezi wa haki za binadamu, duniani kote.


Tamko lake kwamba gereza la Guantanamo litafungwa mara atakapoingia madarakani , linaleta matumaini, kama alivyo yeye binafsi, ambapo kwa muda wa karne mbili watu wa asili ya Afrika walikumbana na ubaguzi wa rangi pamoja na utumwa.


Hadi sasa uchunguzi huu wa shirika la Human Richt Watch unavunja moyo kuliko kuleta matumaini. Katika nchi zaidi ya 90 duniani bado watu wanafanyiwa mateso na serikali, vyombo vya dola vya upelelezi ama makundi ya kijamii, kwa jina la kutofautiana kidini ama kubughudhiwa.


Iwapo ni nchini Cuba ambako wapinzani wa serikali wamewekwa kizuizini kama wafungwa wa kisiasa, ama nchini Iran ambako viongozi wa kidini huwafanyia mateso wanawake na watoto ama Burma ambako watawa ambao wanaoipinga serikali pamoja na watu wengine wanaowaunga mkono , maandamano yao yalikandamizwa kikatili na watawala wa nchi hiyo.


Katika jumla ya mataifa ambayo hadi sasa yanatekeleza hatua za mateso, kama ilivyo katika gereza la Guantanamo, Marekani pia imo, inajiunga pia na mataifa yenye ushawishi kama Urusi, India na China na ambayo yanatoa picha mbaya ya kuwa pamoja katika matendo ya mateso na kuteteana katika umoja wa mataifa. Ripoti hiyo inaitaja Urusi kutokana na suala la Uzbekistan , Afrika kusini kutokana na suala la utawala wa rais Mugabe nchini Zimbabwe na China kutokana na suala la utetezi wake kwa Sudan kuhusu suala la Darfur na Burma.

►◄
 • Tarehe 15.01.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GYnS
 • Tarehe 15.01.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GYnS
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com