Haki za Binadamu nchini China kabla olimpik | Michezo | DW | 08.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Haki za Binadamu nchini China kabla olimpik

China imeanza kukodolewa macho na kukumbushwa ahadi ilizotoa za kuheshimu haki za binadamu na kutoa uhuru wa vyombo vya habari pale ilipochaguliwa kuandaa michezo ya 2008.

Kuchaguliwa kwa China kuandaa michezo ya olimpk kuliambatana na jukumu iliojitwika kuboresha haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari nchini hadi itakapofunguliwa michezo hiyo August 8,mwakani. Je, China inatimiza jukumu hilo ?

Mwaka kabla michezo ya 29 ya olimpik ya majira ya kiangazi kufunguliwa rasmi,haioneshi kwamba China itatimiza jukumu hilo.

Ndio,masharti ya kufanya kazi kwa waandishi habari wa kigeni yametengenea kiasi Fulani lakini yale ya maripota wa nyumbani China yangali ni magumu kama zamani na wanadhibitiwa na vyombo vya dola.Waandishi habari 29 wamekamatwa na wawili wako korokoroni tangu robo-karne .Hii ni rekodi ya dunia ya kuhuzunisha.

Sura sawa na hiyo inaonekana katika sekta ya haki za binadamu na za kiraia:Yule ambae anaethubutu nchini China kufungua mdomo wake na kutaja maovu yanayopita,huyo anajihatarisha kutiwa nguvuni au kuwekwa kizuizini nyumbani.Na hata kulamkomoto.

Vitisho ndio silaha ndogo kabisa.Mabosi wa mikoa huwaajiri majambazi wanaopiga watu ili kuwanyamazisha wakosoaji wa serikali.Hawajali iwapo wakosoaji walengi mashtaka yao dhidi ya chama-tawala cha kikoministi bali wanadai usafi wa mazingira –jambo ambalo hata serikali yenyewe inapigana kuboresha.

Yasikitisha kusikia kila kukicha vilio vya machine wengi wanaolalamika juu ya dhulma,rushua na ukosefu wa sheria.Taasisi pekee ambayo China inaisikiliza wakati huu ni Halmashauri Kuu ya olimpik Ulimwenguni-IOC.Lakini hata nayo muda mrefu sasa imefumba macho na masikio.

Yafaa kutumai kuwa rais wa Halmashauri hiyo ya olimpik Jacques Rogge hafikirii tu fedha nyingi halmashauri yake itavuna kutoka michezo hii,bali pia IOC itaangalia upande wapili wa medali za dhahabu,fedha na shaba.Yafaa pia kutumai wanaolimpik katika vikao vyao na mashirika yanayotetea haki za binadamu watasikiza mapendekezo yao kwa wanasiasa wa China.

Maswali hayo yote mwaka kabla bunduki kulia kuanzisha michezo ya olimpik majibu yake si wazi.Mashirika ya haki za binadamu alao huko Hongkong, yanaweka matumaini kidogo kwamba baada ya dhiki si dhiki,bali faraji.

Katika taarifa rasmi za serikali ya China yanachapishwa maoni ya wakereketwa wa haki za binadamu.Ikiwa huu ni mwanzo wa kuregezwa kamba ,hakuna ajuwae. Kwani China mara nyingi hupiga hatua moja mbele na mbili nyuma.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com