1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haaland aizima RB Leipzig

10 Januari 2021

RB Leipzig imepoteza nafasi ya kuongoza jedwali la ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga baada ya kupokea kichapo cha 3-1 na Borussia Dortmund.

https://p.dw.com/p/3njxZ
Deutschland Bundesliga RB Leipzig - Borussia Dortmund | Haaland
Picha: Ronny Hartman/REUTERS

Mabao ya Dortmund yalitiwa wavuni na Jadon Sancho na Erling Halaand aliyefunga mabao mawili. Bao la kufutia machozi la Leipzig lilifungwa na Alexander Sorloth.

Nayo klabu ya Schalke imepata ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuilemea TSG Hoffenheim kwa mabao manne bila jawabu 4-0.

Mchezaji wa Schalke Mathew Hoppe alifunga mabao matatu "hetriki" huku bao la nne likifungwa na Amine Harit.

Kufuatia matokeo hayo ya wikendi, Bayern Munich bado iko kileleni mwa Bundesliga ikiwa na alama 33 licha ya kupoteza mechi yao dhidi ya Borussia Mönchengladbach, RB Leipzig ni ya pili na alama 31, Bayer Leverkusen ni ya tatu ikiwa na 29 alafu Borussia Dortmund imetulia katika nafasi ya nne na alama 28.

Mechi za mzunguko wa 16 za Bundesliga zitachezwa tena kuanzia Ijumaa ya 15.01.2021 kati ya FC Union Berlin na Bayer Leverkusen.