1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Amerika kusini na karibiki ni kitovu cha COVID-19

Sekione Kitojo
10 Julai 2020

Mataifa ya Amerika kusini na karibiki yamekuwa kitovu cha janga la COVID-19, ambapo nchi kadhaa sasa zina idadi kubwa ya maambukizi kwa jumla ya idadi ya watu wa nchi hizo na idadi ya juu ya  kesi za maambukizi duniani.

https://p.dw.com/p/3f4xQ
Antonio Guterres PK Covid-19
Picha: webtv.un.org

Hayo  yamesemwa na  katibu  mkuu  wa  Umoja  wa  Mataifa Antonio Guterres jana  alipotoa  ujumbe  kwa  njia  ya  vidio  na kusema  kunywea  kwa  pato jumla  la  taifa GDP kunatarajiwa mwaka  huu  katika  eneo  hilo,  ambalo litakuwa  kubwa  zaidi  katika kipindi  cha  karne moja.

Antonio Guterres PK Covid-19
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumzia kuhusu athari za janga la COVID-19 na kutoa wito wa kusitishwa mapigano dunianiPicha: webtv.un.org

"COVID-19 inawakilisha  mshituko  mkubwa  wa  kiafya, kijamii  na kiuchumi  utakaoambatana na  matatizo  makubwa  ya  kiutu katika nchi  za  Amerika ya kusini  na  visiwa  vya  Karibiki," ripoti ya Umoja wa  Mataifa  imesema.

Hali  hiyo inatarajiwa  kusababisha  mdororo  mkubwa  kabisa  wa kiuchumi katika  enzi  hizi.

Kwa mujibu  wa  ripoti hiyo ya  Umoja  wa  mataifa, ukosefu  wa  ajira katika  kanda  hiyo  ya  Amerika kusini unatarajiwa  kupanda  hadi asilimia  13.5  kutoka  asilimia  8.1  mwaka  jana, ukiathiri zaidi  ya watu  milioni  44, ikilinganishwa  na  zaidi  ya  watu milioni  18 mwaka 2019. Kiwango  cha umasikini kinatarajiwa  kupanda  hadi  asilimia 37.2 kutoka  asilimia  30.2, ikiwa  na  maana  watu milioni  230 wataathirika  ikilinganishwa  na  watu  milioni 185  mwaka  jana , taarifa  hiyo  imesema.

Singapur Wahlen 2020
Watu wanaoishi na ulemavu katibu mkuu amesema wako dhaifu kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19Picha: picture-alliance/AP Photo/R. Chan

Hali mbaya Latin Amerika

Guterres  alisema  Amerika  kusini  na  visiwa  vya  Karibiki tayari zinakabiliwa na, "hali  mbaya ya kutokuwa na  usawa," viwango  vya juu  vya  ajira  ambazo  si rasmi  na  huduma  mbovu  za afya, na watu ambao wamo  katika  hatari  kubwa  katika  kanda  hiyo" kwa mara  nyingine  tena  wanaathirika  kwa  kiwango  kikubwa " na COVID-19

"Wanawake, wazee, watu wenye ulemavu, jamii ya watu wa asili, watu wenye asili  ya  Afrika, pamoja  na  wahamiaji  na wakimbizi," pia wanateseka kwa kiwango  kikubwa, wakati  hali mbaya ikiongezeka."

Wakati  huo huo zaidi ya  kesi 60,500  za  maambukizi  mapya zimeripotiwa  nchini  Marekani  hadi jana, kwa  mujibu wa hesabu iliyowekwa  pamoja  na  shirika  la  habari la  Reuters, ikiwa  weka rekodi  ya  maambukizi  ya  siku  moja  wakati Wamarekani wenye hofu wakiambiwa  wachukue tahadhari zaidi na janga  hilo litumiwa kisiasa zaidi.

Deutschland Corona-Pandemie Symbolbild Mundschutz beim einkaufen
Licha ya shughuli kufunguliwa nchini Ujerumani bado maambukizi yanaongezekaPicha: Imago Images/Xinhua/Binh Truong

Nchini Ujerumani  idadi ya kesi  za maambukizi zilizothibitishwa zimeongezeka  kwa watu 395 hadi  watu 198,178, data  kutoka taasisi  ya  kuzuwia  magonjwa  ya  Robert Koch zimeonesha  leo.

Nae waziri  wa  uchumi  wa  Japan amesema  leo kuwa  hatua  mpya zinahitajika  kuzuwia  kusambaa kwa maambukizi  ya  virusi  vya corona  katika vilabu vya usiku  na  mabaa, ambavyo vimeonekana sasa  kuwa  ni  chanzo cha  maambukizi.