Guinea ya Ikweta yamtimua kocha wa taifa | Michezo | DW | 02.01.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Guinea ya Ikweta yamtimua kocha wa taifa

Wenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Guinea ya Ikweta wamemtimua kocha Andoni Goikoetxea ikiwa ni wiki tatu tu kabla ya kuanza dimba hilo, hali inayoyatumbukiza maandalizi yao katika mparaganyiko

Goikoetxea aliondoka Alhamisi baada ya uchaguzi wa kiongozi mpya wa Shirikisho la Kandanda la Guinea ya Ikweta (FEGUIFUT) wiki iliyopita. Rais mpya wa FEIGUFUT Andres Jorge Mbomio amethibidha kupigwa kalamu kocha huyo mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uhispania, ambaye amekuwa usukani kwa miaka miwili iliyopita, lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu uamuzi huo.

Guinea ya Ikweta ambayo ilipewa kibali cha kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya nchi 17, baada ya Morocco kujiondoa kutokana na hofu ya ugonjwa wa Ebola, itacheza dhidi ya Congo katika mechi yake ya ufunguzi ya mashindano hayo mjini Bata mnamo Januari 17.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Gakuba Daniel

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com