1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GUATEMALA: Mji wa Sochi kuandaa mashindano ya Olympics

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlq

Mji wa mapumziko wa Sochi nchini Urusi jana ulishinda haki ya kuandaa mashindano ya michezo ya Olympics ya msimu wa baridi mwaka wa 2014 baada ya rais wa Urusi, Vladamir Putin kufaualu kuishawishi kamati ya kimataifa ya Olypmic, IOC.

Rais wa kamati hiyo, Jacquea Rogge alitangaza ushindi wa mji wa aSochi wakati wa sherehe zilizofanywa mjini Guatemala.

Mji wa Sochi ukigombea kwa mara ya kwanza kuyaandaa mashindano hayo, uliushinda mji wa Pyeongchang wa Korea Kusini kwa kura 51 kwa 47 ingawa maeneo yote 11 yaliyopendekezwa kufanyiwa michezo hiyo hayajajengwa.

Hapo awali kamati ya kimataifa ya Olypic ilieleza wasiwasi wake kuhusiana na ujenzi wa maeneo hayo na swala la mazingira.