Guardiola kuchukua usukani Manchester City | Michezo | DW | 02.02.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Guardiola kuchukua usukani Manchester City

Sasa ni rasmi kuwa Mhispania Pep Guardiola ndiye kocha mpya wa Manchester City katika msimu mpya wa 2016/2017. Guardiola ametia saini mkataba wa miaka mitatu na miamba hao wa ligi ya Premier

Guardiola, atachukua majukumu hayo kuanzia Julai, klabu hiyo ya Ligi ya Premia imetangaza. Manuel Pellegrini ataondoka klabu hiyo Juni 30 baada ya kumalizika kwa msimu wa huu.

Taarifa ya Man City imesema, "Kutokana na heshima yetu kwa Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu ingependa kufanya wazi uamuzi wake ili kuondoa nafasi ya uvumi,”

Manchester City imekamilisha majadiliano na Pep Guardiola na sasa imeshatia sahihi kandarasi na kocha huyo kuchukua hatamu msimu ujao wa 2016/17. "Manuel, ambaye anaunga mkono kikamilifu uamuzi wa kufanya tangazo hili, anaangazia kutimiza malengo yake ya msimu huu na anadumisha kujitolea na heshima ambayo amekuwa nayo machoni ma wote wanaohusika katika uongozi wa klabu.”

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Sessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com