GUARATINGUETA : Papa aendelea na ziara Brazil | Habari za Ulimwengu | DW | 13.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GUARATINGUETA : Papa aendelea na ziara Brazil

Papa Benedict ameendelea na ziara yake nchini Brazil kwa kutembelea kituo cha tiba ya waathirika wa madawa ya kulevya katika eneo la kusini mashariki ya nchi hiyo.

Maelfu ya watu walikusanyika kumlaki Papa.

Kituo hicho kilichopewa jina la Shamba la Matumaini kimeasisiwa na mtawa wa kiume wa Ujerumani na kinasema kimefanikiwa kwa asilimia 80 kuwatibu waathirika wa madawa ya kulevya.Kituo hicho kinatowa muongozo wa kiroho katika kuwatibu waathirika hao wa madawa ya kulevya na kuwafunza kuingia katika ulimwengu wa kazi.

Papa leo atakuwa na misa ya hadhara katika mji wa Aparecida na mkutano wa wazi na maaskofu wa Amerika ya Kusini na Caribbean.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com