1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GUANTANAMO BAY: Maandamano kufanywa dhidi ya gereza la Marekani la Guantanamo.

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbp

Maandamano yamepangwa kufanywa katika maeneo mbalimbali duniani kupinga gereza la Marekani la Guantanamo liloloko Cuba.

Maandamano hayo yatafanyika miaka mitano tangu gereza hilo, ambalo lina wafungwa takriban mia nne washukiwa wa ugaidi, lilipoanzishwa.

Marekani inawachukulia baadhi ya wafungwa hao kuwa maadui wa kivita na hivyo kuwanyima haki nyingi za kimsingi, kulingana na sheria za kimataifa.

Hatua hiyo ya Marekani imesababisha upinzani mkali mara kwa mara kutoka kwa makundi ya kuetetea haki za binadamu.