1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gotze: Sifikirii kuhusu nafasi yangu kwenye Kombe la Dunia

30 Juni 2022

Mshindi wa Kombe la Dunia Mario Goetze hafikirii kuhusu kurejesha nafasi yake katika timu ya Ujerumani kabla ya Kombe la Dunia la Qatar haswa baada ya kurejea Bundesliga akiwa na klabu ya Eintracht Frankfurt.

https://p.dw.com/p/4DSkf
Fußball Bundesliga Dortmund Wolfsburg Flash-Galerie
Picha: dapd

Mario Goetze, kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 30, ambaye alifunga bao la ushindi katika fainali ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Argentina, alisaini mkataba na mabingwa wa Ligi ya Europa Eintracht wiki iliyopita baada ya miaka miwili akiwa na klabu ya PSV Eindhoven.

Alirejea tena katika ubora wake katika klabu hiyo ya Uholanzi kufuatia uhamisho wake wa 2020 kutoka Borussia Dortmund, na kusababisha uvumi kuhusu uwezekano wa kurejea katika timu ya taifa kwa wakati katika Kombe la Dunia baadaye mwaka huu.

Goetze alipokea ujumbe wa pongezi kutoka kwa kocha wa Ujerumani Hansi Flick kwa uhamisho wake kwenda Eintracht lakini akasema Kombe la Dunia sio suala lenye umuhimu kwake.

"Jambo muhimu zaidi ni kuimarika na kushinda nikiwa na timu. Mengine yatakuja," Goetze aliwaeleza waandishi wa habari siku ya Jumanne. Mechi yangu ya mwisho ya kimataifa ilikuwa miaka michache iliyopita (2017). Wakati huo nilikuwa na jukumu maalum na yote yalikuwa karibu nami. Kwa sasa, hilo sio suala la muhimu kwangu."

Eintracht watashiriki katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao wakiwa washindi wa Ligi ya Europa.

Kombe la Dunia litafanyika Novemba na Desemba nchini Qatar.

Goetze aliongeza kuwa "nia yangu iko kwenye  klabu yangu  kupata manufaa zaidi kutokana na uchezaji wangu. Mengine yote hayapo kichwani mwangu kwa sasa, kwa sababu si mambo yenye umuhimu katika siku zijazo."

Kiungo huyo mshambuliaji, ambaye alianza soka lake huko Dortmund kabla ya kujiunga na Bayern Munich kwa kipindi cha miaka mitatu mwaka 2013 na kisha kurejea Dortmund. Ligi ya Bundesliga itaanza Agosti 5 kwa Eintracht kumenyana na mabingwa Bayern