Global Media Forum 2014 | Masuala ya Jamii | DW | 14.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Global Media Forum 2014

Kongamano la kila mwaka la DW ambalo linawaleta pamoja wataalamu kutoka vyombo vya habari, wanasayansi na wanasiasa litafanyika kuanzia tarehe 30 Juni mpaka tarehe 2 Julai 2014

Tovuti (World Wide Web) imekuwa msingi wa mawasiliano ya dunia, katika nyanja za uchumi, sayansi na siasa. Imefungua mlango kwa mamilioni ya watu na kuwapa fursa ya kushiriki katika masuala ambayo yako mbali ya mipaka ya jamii zao. Enzi ya digitali imeleta fursa, lakini pia inaambatana na hatari. Matumizi mabaya ya internet yanatokea katika mitindo mbali mbali, kama vile uhalifu wa kimtandao, na kupambana na changamoto hizo kunahitaji juhudi za pamoja kati ya watunga sera na makampuni ya biashara. Deutsche Welle inatarajia kuwa watu zaidi ya 2000 watashiriki kwenye mjadala kuhusu suala hili.
Bonyeza hapa kupata maelezo mengine: www.dw.de/globalmediaforum

Viungo vya WWW

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com