1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Glasgow, Scotland. Chama kinachotaka uhuru chapata ushindi.

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4i

Nchini Scotland chama kinachotaka uhuru wa jimbo hilo cha Scottish National Party kimepata viti vingi zaidi katika bunge la nchi hiyo, na kukishinda kwa kiasi kidogo chama cha Labour cha waziri mkuu anayeondoka madarakani Tony Blair.

Chama cha SNP kimepata viti 47 dhidi ya viti 46 ilivyopata Labour.

Chama cha Conservative kimepata viti 17.

Matokeo hayo yanafikisha mwisho muungano wa hapo kabla wa chama cha Labour nchini Scotland pamoja na chama cha Leberal Democrats. Kiongozi wa chama cha SNP Alex Salmond anaweza kuwa waziri wa kwanza mkuu. Katika matokeo mengine katika uchaguzi wa majimbo nchini Uingereza, chama cha Labour kimepoteza udhibiti jumla katika bunge la Wales. Wachunguzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa inawezekana kuunda muungano na Waliberali. Nchini Uingereza chama cha kihafidhina kilichoko katika upinzani kimepata mafanikio machache lakini si kama ilivyotarajiwa.