1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GHAZNI:Taleban na Afghanistan watafuta mahali kwa mazungumzo ya ana kwa ana

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcE

Serikali ya Afghanistan na wateka nyara wa kundi la Taleban hii leo wanajadiliana mahali pa kufanyika mazungumzo ya ana kwa ana juu ya kuachiwa kwa mateka 21 wa Korea Kusini wanaoshikiliwa zaidi ya wiki mbili sasa na kundi hilo la Taleban.

Ujumbe wa Serikali ya Korea Kusini ulikuwa katika jimbo la Ghazni Kusini Magharibi mwa Kabul wanakoshikiliwa mateka hao, kujaribu kutafuta uwezekeno wa kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana.

Kundi hilo la Taleban linataka mazungumzo hayo yafanyike kwenye eneo lililochini ya himaya yao na wamehakikisha usalama kwa ujumbe wa Serikali ya Korea Kusini.

Vinginevyo msemaji wa kundi hilo amesema kuwa, vikosi vya usalama vya umoja wa mataifa vilinde usalama katika eneo lingine litakalopendekezwa.

Wakati huo huo msemaji wa Polisi katika jimbo hilo amesema kuwa wamefanikiwa kupeleka madawa kwa ajili ya mateka wanawake 18 na wanaume wawili, lakini watekaji hao wamekataa ombi la serikali ya Afghanistan kupeleka madaktari kuwatibu mateka.

Tayari watekaji hao wamekwishawaua mateka wawili kati ya 23 iliyowateka.