1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GHAZNI:Madai ya Taleban ya kuachiwa wafungwa wao kutimizwa

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcb

Maafisa wa Korea Kusini bado wanajaribu kujadiliana na kundi la Taleban ili kuwashawishi kuwaachia huru mateka 21 wanaowazuilia.Kulingana na maafisa hao wa serikali madai ya kundi hilo ya muachiwa kwa wafungwa wao walioko jela nchini Afghanistan yatatimizwa.

Mkutano wa ana kwa ana unapangwa kufanyika kati ya maafisa hao na kundi la Taleban baada ya mateka wawili kuuliwa huku wengine waliosalia kutishiwa kifo.

Kulingana na msemaji wakundi la Taleban Yousuf Ahmadi kundi lake liko tayari kufanya mazungumzo na balozi wa Korea Kusini Kang Sung-Zu na wameshachagua wawakilishi wao kuhudhuria kikao hicho.Bado mahala pa kikao chenyewe hapajaamuliwa japo polisi wanasema kuwa patakuwa na ulinzi mkali.

Korea Kusini imekuwa ikijaribu kuishawishi Marekani na Pakistan walio wandani wake kuingilia kati.Shirika la Kutetea haki za Binadamu Amnesty international linatoa wito wa mateka hao kuachiwa.