GHAZNI: Mateka wawili wa Korea Kusini wajiandaa kurejea kwao | Habari za Ulimwengu | DW | 14.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GHAZNI: Mateka wawili wa Korea Kusini wajiandaa kurejea kwao

Wanawake wawili wa Korea Kusini waliotekwa nyara na kundi la Taliban wanajiandaa kuondoka Afghanistan na kurejea nyumbani baada ya kuachiliwa huru.

Msemaji wa kundi la Taliban amesema wanawake hao wameachiwa kama ishara ya ukarimu, baada ya kuwazuilia kwa zaidi ya wiki tatu.

Wanamgambo wa Taliban bado wanawazuilia mateka 19 wa Korea Kusini. Tayari kundi hilo limewaua mateka wawili likitaka wafungwa wa Taliban waachiliwe huru kutoka gerezani.

Wakati huo huo, mwanamume aliyejitambulisha kuwa mjerumani anayeshikiliwa na Taliban nchini Afghanistan amesema kwa njia ya simu kwamba watekaji nyara wametishia kumuua.

Haijathibitishwa ni nani aliyepiga simu hiyo kwa chombo kimoja cha habari, lakini wizara ya mashauri ya kigeni ya Ujerumani imesema maafisa wake wanaendelea na juhudi za kumuokoa raia huyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com