Ghana ina miadi na Brazil mwezi huu. | Michezo | DW | 14.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ghana ina miadi na Brazil mwezi huu.

Kombe la Ulaya la UEFA linarudi uwanjani na timu 2 za Ujerumani-Bremen na Leverkusen zikigombea tikiti za robo-finali.Ghana itacheza na Austria na Brazil.

Uwanjani jioni hii ni duru ya pili ya kutoana ya kombe la UEFA-kombe la shirikisho la dimba la Ulaya.Timu 2 za Ujerumani: Werder Bremen na Bayer Leverkusen zitakuwa uwanjani.

Ghana –Black stars- ina miadi na Brazil-marudio ya changamoto yao ya kombe lililopita la dunia ?

Argentina imeipiku Itali- mabingwa wa dunia katika orodha ya mwezi uliopita ya timu bora za dunia na Kenya leo ina miadi na Kanada huko St-Lucia,Caribbean katika kombe la dunia la Cricket.

Katika kinyan’ganyiro cha jioni hii cha Kombe la Ulaya la UEFA,Werder Bremen wanatokwa na jasho wakati huu kwa kuwa hawana uhakika iwapo jogoo lao usoni Miroslav Klose litakuwa fit kuteremka uwanjani au la.Bremen iliizaba Celta Vigo ya Spain katika duru iliopita bao 1:0 huko Spain na leo ikicheza nyumbani,inataka kulizuwia jogoo la shamba kuwika mjini.Klose amekuwa akipewa matibabu kuondoa maumivu yake ya mgongo.

Mshambulizi wao Hugo Almeida aliewapatia bao la ushindi dhidi ya Vigo duru iliopita na mchezaji wa kiungo Daniel Jansen pia wanaugua ,lakini kocha wa Bremen Thomas Schaaf, ana matumaini kwamba Bremen leo, itatamba tena mbele ya Celta Vigo .

Akikumbusha mchezo uliopita alisema,

“Nadhani tumecheza uzuri leo.Tumetimiza tuliokusudia.Tumembana adui na nadhani katika kipindi kizima cha dakika 90 na bila shaka kule kutolewa nje kwa mchezaji ,kulitupa sisi nafuu na timu yangu kweli ilitia for a.”

Jioni hii basi kocha Thomas Schaaf hana wasi wasi-Bremen itatamba nyumbani.

Timu nyengine ya Ujerumani inayorudi uwanjani jioni hii ni Bayer Leverkusen ambayo inaumana na Racing Lens ya Ufaransa.

Mkurugenzi wa Bayer Leverkusen,kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Rudi Völler,akikumbusha ushindi wa duru ya kwanza wa mabao 2:1 anasema:

“Tumejionea jionin jana changamoto kali ya kombe la Ulaya.Tulitamba kweli uwanjani lakini kabla ya firimbi ya mwisho bahati mbaya tulitiwa bao nah ii inaumiza.Hatahivyo,mtu ameona kuwa leo tulicheza uzuri zaidi na tuna matumaini mema kuingia duru ijayo.”

Argentina imeparamia kileleni mwa orodha ya FIFA ya timu bora za dimba duniani wakati huu.Hii ni mara ya kwanza kukalia kiti hicho.Argentina imeipiga kum,bo Itali-mabingwa wa dunia walioangukia mwezi uliopita nafasi ya pili huko Brazil ikiwa nafasi ya 3,Ufaransa ya 4 na Ujerumani ya 5 ikifuatwa na Uingereza.Timu 3 za Afrika zinafuatana katika orodha ya timu bora 20 za dunia:Kamerun iko nafasi ya 18,Ghana ya 19 na Cote d’Iviore au Ivory Coast nafasi ya 20.

Ghana imetangaza majina ya wachezaji 2 wapya kwa timu ya taifa-The Black Stars- kwa mapambano 2 baadae mwezi huu-dhidi ya Austria na Brazil.Wachezaji hao ni nahodha wa timu yao ya olimpik-Michael Helegbe na Alfred Arthur anaeichezea Ashanti-gold.Ghana ndio mwenyeji wa kombe lijalo la afrika la mataifa hapo mwakani na ilicheza na Brazil katika kombe lililopita la dunia hapa Ujerumani.AC Milan ya Itali inamtarajia ronaldinho kujiunga nayo kutoka FCBarcelona msimu ujao.

Huko Ronaldinho atajiunga na wabrazil wengine akina Kaka na Ronaldo.

Bingwa wa zamani wa dunia wa mita 5000 kutoka Kenya, Eliud Kipchoge, ameachwa nje ya timu ya Kenya kwa changamoto ya mwezi huu ya mbio za nyika za dunia-world crosscountry championsship mjini Mombasa.Kipchoge ameonekana si fit kwa zahama za mbio hizo.

Timu ya cricket ya Kenya lakini, ni fit na leo ina miadi na Kanada katika kombe la dunia la Cricket huko St.Lucia katika visiwa vya Caribbean.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com