Geneva. Baraza la haki za binadamu kujadili Darfur. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Geneva. Baraza la haki za binadamu kujadili Darfur.

Kikao maalum cha baraza la umoja wa mataifa la haki za binadamu kuhusiana na maafa yanayowakumba watu wa jimbo la Darfur nchini Sudan kimeahirishwa mjini Geneva hadi leo.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayemaliza muda wake Kofi Annan ametuma ujumbe kupitia video jana Jumanne, akiyataka mataifa 47 wanachama wa baraza hilo kuingilia kati katika kile alichokiita , jinamizi la Darfur kwa kupeleka wachunguzi wao binafsi.

Tangu 2003 zaidi ya watu 200,000 katika jimbo hilo wameuwawa na zaidi ya watu milioni mbili wamekimbia makaazi yao. Serikali ya Sudan inakana kuwapa silaha wanamgambo wa Janjaweed na imekuwa ikisita kukubali jeshi la nyongeza la umoja wa mataifa katika jeshi la umoja wa Afrika. Kamishna wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa, Louise Arbour, amesema raia wanabaki kuwa lengo la mashambulizi ya kinyama kutoka kwa wanamgambo hao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com