GENEVA : Annan asema majeshi ya Marekani yanasa Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GENEVA : Annan asema majeshi ya Marekani yanasa Iraq

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema leo hii kwamba vikosi vya Marekani vimenasa nchini Iraq na kuonya kwamba serikali ya Marekani lazima itafute wakati muafaka wa kuondoka nchini humo bila ya kuitumbukiza nchi hiyo kwenye machafuko makubwa zaidi.

Annan amesema katika suala la kuwepo kwa Marekani kijeshi nchini Iraq ni suala gumu na kwamba wakati wa kuondoka kwake nchini humo hauna budi kuwa unaofaa.

Annan ametahadharisha kwamba kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini kusipelekee kuzidi kwa hali kuwa mbaya nchini humo.

Amesema serikali ya Marekani badala yake inapaswa kujaribu kufikia hali wakati inapoondowa wanajeshi wake wananchi wa Iraq wenyewe wanakuwa na uwezo wa kuidhibiti hali ambayo inahakikisha kuwepo kwa mazingira madhubuti ya usalama.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com