1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gazetini:Mashambulio ya ETA Mallorca

11 Agosti 2009

Nini shabaha yake ?

https://p.dw.com/p/J7YB

Miongoni mwa mada za ndani na nje ya Ujerumani zilizochambuliwa leo kwa mapana na m arefu na wahariri wa magazeti ya Ujerumani,ni kufikishwa mahkamani jana kwa kile kinachitwa "kikundi cha Sauerland" hapa Ujerumani-kikundi cha magaidi waliotiwa nguvuni kwa kupanga njama ya kushambulia kambi ya kijeshi ya wamarekani humu nchini.Mada nyengine ni hujuma za magaidi wa ETA nchini Hispania zinazolengwa kuchafua biashara ya utaliii kisiwani Mallorca.

Gazeti la Allgemeine Zeitung kutoka Mainz juu ya kundi la Sauerland :

Washtakiwa wana azma gani kuungama makosa yao? Lauliza gazeti.Je, kufanya hivyo madhumuni yao ni kupunguziwa adhabu ?-gazeti lajibu la,wasitarajie hivyo.Au wanataka kusaidia idara za ulinzi za Ujerumani ? gazeti pia lajibu hapo kuwa hiii pia haiyumkiniki.ikiwa ni hivyo, wataka nini ? lauliza gazeti.

Linadhani kwamba kwa kuungama madhambi yao wanataka kuchochea hofu na kihoro katiika jamii.Wanataka kusema angalieni kile tunachoweza kufanya.Si taabu kwetu kuwasajiili vijana,kuwapa mafunzo na kuwatuma kutekeleza hujuma za kigaidi.Hakika ni kuwa hatari ya ugaidi imesalia kuwapo hata nchini Ujerumani.Kuingiwa na hofu kubwa kuna dhara.Kwamba yawezekanya kuzima njama ya kigaidi kabla kutokea,kikumndi cha Sauerland kimetoa mfano.

Hilo ni Allgemeine Zeitung kutoka mjinii Mainz.

Ama gazeti la Osnabrucker Zeitung linahisi kuungama kwa Fritz Gelowitcz katika kesi ya gengii hili la sauerland,yapasa kuzushe wasi wasi mkubwa hasa kumuona akielezea biila wasi wasi njama waliopanga ya mauaji kwa jina la Allah. Gazeti laongeza:

"Mtoto huyu wa mwanabiashara kutoka ulm aliejitenga kabisa na jamii ya kijerumani ili kuutumikia uislamu na kama kipofu kuihujumu jamii hiyo.Aliyosema yanatisha kwa kubainisha wazi kuwa ugaidi wa kiislamu zamanii umetia shina humu nchini mwetu.Gelowicz na wenzake 3,2 wajerumani waliosiilumu pamoja na 2 wa asili ya kituruki waliazimia kuashamoto mkubwa nchini mwao."

Likitugeuzia mada ,gazeti la "DER NEUE TAG" linasema hali ya wasi wasi wa kuripuka kwa mabomu hiivii sasa miongoni mwa watalii huko Mallorca,Hispania imechukua sura mpya.gazeti laongeza:

"Baada ya mripuko 4 wa bomu mwishoni mwa wiki, hata watalii walevi wakubwa wa pombe ,wamepata habari zao .Kwani, chama cha magaidi cha ETA kinahujumu sasa shiina la biashara ya utalii ya Hispaniia na kwa kufanya hivyo kinajifanya kutengwa zaidi....kwanii hata katika jimbo la Baske zamani imefahamika kwamba linajiendesha wenyewe katika mambo yake ya ndani na kwamba linanufaika mno na uwanachama wa Spain katika Umoja wa Ulaya.

Mod.Braunschweiger Zeitung linadai kwamba hujuma za kigaidi za chama cha ETA kamwe hadi sasa hazikufaulu kuzuwia biashara ya utalii nchini Hispania.Lakini kuiangalia sura ya mambo kwa jicho la kiuchumi tu hgaitoshi.Gazeti laandika:

..........Ni makosa kutegemea kuwa hata siku zinazokuja kila kitu kitakwenda uzuri.Kwani , hakuna awezae kusema kwa uhakika,kuwa ETA haitafanya hujuma ya kikatili kama ile ya Palmanova.Na hakuna aneweza kuondoa uwezekano kuwa bomu laweza likaripuka kwa makosa tu kabla simu kupigwa kuonya.

Muandishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman