GAZA:Wanajeshi wa Israel waondoka beit Hanoun lakini wamewauwa wapalestina wengine 7 akiwemo mwanamke | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Wanajeshi wa Israel waondoka beit Hanoun lakini wamewauwa wapalestina wengine 7 akiwemo mwanamke

Vikosi vya Israel vimeondoka kwenye mji wa Beit Hanoun kaskazini mwa Ukanda wa Gaza baada ya opresheni ya muda mrefu iliyosababisha kuuwawa kwa wapalestina 50 na mwanajeshi wa Israel.

Kwa mujibu wa maafisa wa Israel Opresheni hiyo ililengwa kukomesha mashambulio ya Roketi ya wanamgambo wakipalestina dhidi ya Israel.

Hata hivyo muda mfupi baada ya wanejshi hao wa Israel kuondoka kwenye eneo hilo la Beit Hanoun wanamgambo wa Palestina walivurumisha roketi ndani ya Israel katika mji wa Ashkelon.

Wakati huo huo vikosi vya Israel vimeripotiwa kuwauwa wapalestina 7 waliokuwa na sialaha pamoja na mwanamke mmoja katika operesheni ya iliofanywa na na wanajeshi hao katika maeneo mengine matatu huko kaskazini mwa Gaza.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com