GAZA:UN yaonya kutokea tena maafa | Habari za Ulimwengu | DW | 29.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:UN yaonya kutokea tena maafa

Umoja wa Mataifa umeonya kutokea kwa madhara mengine huko Ukanda wa Gaza siku moja baada ya watu watano kufa kufuatia kuta za bwawa la maji machafu kupasuka na kupelekea mafuriko.

Mkuu wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa huko Gaza John Ging amesema kuwa sehemu kubwa ya kuta za bwawa lingine zinakaribia kupasuka.

Waokoaji wanaendelea na juhudi za kutafuta miili ya watu wengine inaohisiwa wamekufa.

Katika tukio lingine watu wasiyofahamika waliyokuwa na silaha walilifyatulia risasi gari la kamanda wa kundi la Hamas huko Gaza, ambapo mke na watoto wawili wa kamanda huyo walijeruhiwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com