GAZA:Mapigano kati ya Israel na Palestina yaendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 22.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Mapigano kati ya Israel na Palestina yaendelea

Israel na wapiganaji wa kipalestina wamendelea kurushiana makombora, katika siku ya tatu ya mapigano kati ya pande hizo.

Wapalestina watano na mwanamke mmoja wa Kiisrael wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni.

Mwanamke huyo aliuawa baada ya roketi kurushwa na kuangukia gari lake katika mji wa kusini mwa Israel wa Sderot, ikiwa ni mara ya kwanza kwa makombora ya kipalestina kusababisha madhara kwa Israel toka mwezi Novemba mwaka jana.

Mapema hapo jana Israel ilifanya mashambulizi makali ya anga na kuwaua wapiganaji wanne wa kundi la Jihad.

Baraza la Usalama la Israel lilikubaliana hapo siku ya Jumapili kuendelea na mashambulizi dhidi ya Palestina ikiwa ni katika kujibu mashambulizi ya makombora kiasi cha 150 yaliyovurumishwa kutoka Gaza toka wiki iliyopita.

Waziri wa miundo mbinu ya kitaifa wa Israel Binyiman Ben-Eliezer amesema kuwa ni lazima wawaangamize viongozi wa wanamgambo hao wa kiislam.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com