1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza: Waziri Mkuu wa Palestina atoa wito mzozo Lebanon umalizwe kisiasa.

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtY

Waziri Mkuu wa wapalestina, Ismail Haniya, ameitaka Lebanon ikubali kushauriana na wanamgambo wa Kiislamu ili kumaliza vita kati ya wanamgambo hao na wanajeshi wa nchi hiyo.

Kiongozi huyo wa chama cha Hamas amesema mzozo huo unapaswa kumalizwa kisiasa wala si kwa matumizi ya nguvu za kijeshi.

Ismail Haniya amesema kambi kumi na mbili za wakimbizi wa kipalestina nchini Lebanon zinapaswa kuwa hifadhi salama.

Kiasi watu mia moja kumi na watano wameuawa katika mapigano kati ya wanamgambo wa Fatah al-Islami na majeshi ya Lebanon.

Mashirika ya kutoa misaada yana wasiwasi kuhusu hatma ya raia kiasi elfu nne wa kipalestina walionaswa katika kambi ya Nahr al-Bared karibu na mji wa bandari wa Tripoli, kaskazini mwa nchi hiyo.