Gaza. Wapalestina wauwawa na jeshi la Israel. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Wapalestina wauwawa na jeshi la Israel.

Wapalestina saba wameuwawa katika mashambulio kadha ya anga yaliyofanywa na jeshi la Israel yakiwalenga wapiganaji katika ukanda wa Gaza.

Watatu kati ya waliouwawa wakati gari yao iliposhambuliwa kwa bomu katika mji wa kaskazini wa Khan Yunus walitambuliwa kuwa wanachama waandamizi wa kundi la wapiganaji wa Islamic Jihad.

Shambulio la pili dhidi ya kambi ya wakimbizi katikati ya Gaza limesababisha vifo vya wapiganaji wawili wa kikosi cha mashahidi wa Al Aqsa, kundi la wapiganaji linalohusishwa na chama cha rais Mahmoud Abbas cha Fatah.

Watu wawili waliokuwa karibu pia wameuwawa katika shambulio hilo.

Kiasi Wapalestina wengine watano wamejeruhiwa katika shambulio la anga la Jumamosi, ambalo lilifanyika kufuatia shambulio la kombora dhidi ya Israel lililorushwa kutoka Gaza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com