GAZA: Wanamgambo wa Hamas watishia kushambulia vituo vya Fatah | Habari za Ulimwengu | DW | 12.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Wanamgambo wa Hamas watishia kushambulia vituo vya Fatah

Wanamgambo wa Kipalestina wa tawi la kijeshi la Hamas,wametishia kushambulia vituo vya usalama vya kundi hasimu la Fatah mjini Gaza.Misikiti inayoongozwa na Hamas katika mji wa Gaza,imewapa wanamgambo wa Fatah muda wa saa mbili kuondoka kwenye vituo vyao.Ripoti za vyombo vya habari zinasema,wanamgambo wa Hamas wameshaanza kuvamia vituo vingine vya Fatah vilivyo kaskazini na kati kati ya Gaza.Wakati huo huo,chama cha Fatah kinachoongozwa na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas kimesema,kitaamua ikiwa kijitoe kwenye serikali ya umoja iliyoundwa pamoja na Hamas miezi mitatu iliyopita.Hatua hiyo inafauatia vifo vya watu 16 kwenye mitaa ya Gaza,katika muda wa saa 24 zilizopita,licha ya kuwepo makubaliano ya kuweka chini silaha tangu Jumatatu usiku.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com