1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wanamgambo wa Hamas na Fatah wapambana upya

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVQ
Mtoto wa wakimbizi huko Angola
Mtoto wa wakimbizi huko AngolaPicha: AP

Mapambano kati ya makundi hasimu ya Kipalestina yameendelea kwenye Ukanda wa Gaza.Si chini ya watu 5 walijeruhiwa katika machafuko mapya yaliyozuka kati ya wanamgambo wa Hamas na Fatah licha ya makundi hayo kukubali kuweka chini silaha zao.Siku ya Ijumaa,si chini ya watu 20 waliuawa katika mapigano ya makundi hayo mawili.Wajumbe wa chama tawala Hamas na wa chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas,wanatazamiwa kukutana tena kujaribu kukomesha mapigano. Miripuko ikitikisa mji wa Gaza,shule na maduka yamefungwa na wakazi wanajificha majumbani mwao. Mapigano mengine pia yameripotiwa Beit Lahiya upande wa kaskazini na hata Khan Yunis kusini mwa Gaza.Wakati huo huo,Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia,amewahimiza rais Abbas na kiongozi wa Hamas,Khaled Meshaal kukutana Jumanne ijayo mjini Mecca.