1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Vyama vya wapalestina vyaendelea kupigana.

14 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBri

Wanamgambo wa chama cha Hamas wamekiteka kituo muhimu cha kiusalama cha wapiganaji wa Fatah katika ukanda wa Gaza.

Watu walioshuhudia wanasema wanamgambo hao waliwaburura wapiganaji wa Fatah waliojisalimisha kutoka jumba moja kisha wakawaua kwa kuwapiga risasi.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, kwa mara ya kwanza amekiagiza kikosi maalum cha ulinzi wa raia kujibu mashambulizi pale kitakaposhambuliwa.

Hata hivyo wapiganaji wa Fatah wanaelekea kuzidiwa nguvu na wanamgambo wa Hamas ambao wana silaha nyingi na bora kuliko Fatah.

Baadaye leo Rais Mahmoud Abbas anatarajiwa kutoa tangazo muhimu litakaoelezea msimamo wa mwisho wa chama chake kuhusu mzozo huo.

Kumekuwa na tetesi kwamba chama cha Fatah huenda kikajitoa kwenye serikali ya muungano wa kitaifa kutokana na mapigano ya hivi karibuni kati ya wanamgambo wa vyama vyote viwili.