1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Rais Abbas ataka mashambulio dhidi ya Israel yakomeshwe

7 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBg

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas leo amewatolea mwito maafisa wake wa usalama wahakikishe mashambulio ya maroketi dhidi ya Israel yanazuiliwa.

Akizungumza katika sherehe za kufuzu kwa walinzi wake, rais Abbas amenukuliwa akisema kwamba ni muhimu kwa pande zote husika kuongeza juhudi, hususan walinzi wa rais na vikosi vya usalama, kudumisha usalama ndani ya mamlaka ya Palestina.

Aidha rais Abbas amesema ipo haja ya kukoma kuvuruga usalama na kuzuia mashambulio ya maroketi dhidi ya Israel yanayovurumishwa kutoka Ukanda wa Gaza.

Sambambana ripoti hizo, waziri wa habari wa Palestina, Mustafa Barghouti, amesema wapatanishi wa Misri wanaofanya juhudi za kuachiliwa huru mwanajeshi wa Israel anayezuiliwa na kundi la wanamgambo wa kipalestina, wamewasilisha orodha ya masharti ya kundi hilo kwa serikali yas Israel.

Waziri Mustafa amesema watekaji nyara hao wanataka Israel iwaachilie huru wafungwa iliyowataja katika orodha yao kabla koplo Gilad Shalit, kuachiliwa huru.

Hata hivyo waziri huyo hakusema ni wafungwa wangapi walio katika orodha hiyo wala kutoa taarifa zaidi.