GAZA: Mpiganaji wa kundi la Hamas auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 22.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Mpiganaji wa kundi la Hamas auwawa

Majeshi ya Israel yameuuwa mpiganaji mmoja wa kundi la Hamas katika shambulio la ndege za kijeshi katika Ukanda wa Gaza.

Watu wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Kundi la Hamas limesema mpiganaji huyo aliyeuwawa ni kamanda wa ngazi ya juu katika kikosi cha Hamas mjini Gaza.

Taarifa ya jeshi la Israel imesema kwamba shambulio hilo lililenga kundi la watu waliokuwa na silaha ambao walikuwa wanaelekea katika sehemu ya mpakani.

Jeshi la Israel katika taarifa yake limewalaumu wapiganaji wa Hamas kwa kuwatumia watoto kwenda kukusanya mabaki ya makombora baada ya mashumbulio.

Hayo yamefuatia pia kuuliwa watoto wawili na raia saba kujeruhiwa katika eneo maalum la kurushia makombora.

Awali jeshi la Israel liliwauwa wapiganaji watatu wa kundi la Islamic Jihad kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com