GAZA : Jordan kuwakutanisha Abbas na Haniyeh | Habari za Ulimwengu | DW | 26.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA : Jordan kuwakutanisha Abbas na Haniyeh

Jordan itakuwa mwenyeji wa mazungumzo kati ya Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wa kundi la Fatah na Waziri Mkuu wa kundi la Hamas kufuatia kuzuka kwa umwagaji damu baina ya makundi yao mawili.

Ghazi Hamad msemaji wa serikali ya Palestina inayoongozwa na kundi la Hamas amesema Haniyeh amekubali mwaliko wa Mfalme Abdullah wa Jordan kuhudhuria mazungumzo hayo na kwamba matayarisho yanafanyika kupanga tarehe ya mazungumzo hayo.

Mvutano kati ya kundi tawala la Hamas na lile la Fatah ambalo huko nyuma lilikuwa likidhibiti Palestina umezuka baada ya Abbas mwezi huu kutowa wito wa kufanyika kwa uchaguzi wa mapema hatua ambayo Hamas wameita kuwa ni mapinduzi ya kuiangusha serikali yake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com