GAZA: Israeli yafanya operesheni ya kijeshi kaskazini mwa ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Israeli yafanya operesheni ya kijeshi kaskazini mwa ukanda wa Gaza

Wizara ya usalama nchini Israeli imesema haikuamrisha operesheni ya sasa hivi ya majeshi ya nchi kavu katika eneo la Ukanda wa Gaza. Hata hivyo, ofisi ya waziri mkuu, Ehud Olmert, imesema shambulio ambalo limanzishwa leo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza litaendelea kukomesha mashambulizi ya makombora ya wapalestina dhidi ya Israeli. Watu 6 wameuawa usiku wa kuamkia leo na wengine 35 wamejeruhiwa na majeshi ya Israeli yakiingia katika mji wa Beit Hanun kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Mashahidi wamesema wanajeshi wa Israeli wakisaidiwa na vifaru vya kijeshi, waliukamata mji huo wa Beit Hanun na kuzuwia njia zote zinazoelekea hospitalini.

Msemaji wa jeshi la Israeli amekiri kuwa kumekuwa kukifanyika operesheni kubwa katika eneo hilo na kwamba mashambulizi mawili ya ndege zao za kivita yamelenga kundi la wapiganaji wakipalestina kiasi ya 30.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com