GAZA : Israel yauwa Wapalestina tisa na kujeruhi kadhaa | Habari za Ulimwengu | DW | 02.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA : Israel yauwa Wapalestina tisa na kujeruhi kadhaa

Vikosi vya Israel vikisaidiwa na vifaru vimeuwa Wapalestina tisa na kujeruhi wengine madarzeni hapo jana katika shambulio kubwa kabisa la Israel kuwahi kushuhudiwa kwa miezi kadhaa katika Ukanda wa Gaza.

Mwanajeshi mmoja wa Israel pia ameuwawa katika shambulio hilo katika mji wa Beit Hanoun ambao hivi sasa unadhibitiwa na Israel.

Operesheni hiyo ni mojawapo ya operesheni kubwa kabisa tokea Israel ilipoanzisha mashambulizi yake kwa Gaza katika kipindi cha kiangazi kilichopia kushinikiza kuachiliwa kwa mwanajeshi wa Israel alietekwa nyara na wanamgambo wa Kipalestina hapo Juni 25 pamoja na kukomesha mashambulizi ya maroketi dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.

Mashambulizi hayo yamelaaniwa na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina na Waziri Mkuu Ismael Haniyeh.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com