Gaza. Israel yaua mpiganaji mmoja katika operesheni Gaza. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Israel yaua mpiganaji mmoja katika operesheni Gaza.

Mashambulizi ya ndege za Israel yamesababisha kiasi mtu mmoja kuuwawa ambaye ni mpiganaji wa kundi la Hamas na kuwajeruhi wengine 10 katika mamlaka ya Palestina leo Jumamosi , wakati jeshi hilo la Israel linaendelea na moja kati ya operesheni yake kubwa kabisa katika ukanda wa Gaza tangu kujiondoa katika eneo hilo mwaka mmoja uliopita.

Mashambulizi hayo mapya yanakuja siku moja baada ya majeshi ya Israel kuwauwa watu 19 wengi wao wakiwa raia, ikiwa ni pamoja na wanawake waliojitolea kuwa ngao ya kibinadamu kati ya majeshi hayo na wapiganaji wa Kipalestina waliojificha katika msikiti

Jeshi la Israel limesema limefyatua risasi dhidi ya wapalestina waliokuwa na silaha , na kwamba operesheni yake katika eneo la Gaza ina lengo la kuzuwia wapiganaji kufanya mashambulizi ya maroketi dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com