GAZA: Israel yaendelea kushambulia Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 22.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Israel yaendelea kushambulia Ukanda wa Gaza

Ndege za kijeshi za Israel zimelenga vituo katikati ya Ukanda wa Gaza.Mashambulizi hayo mapya yamefanywa baada ya wanamgambo wa Kipalestina kurusha makombora katika mji wa mpakani wa Sderot kusini mwa Israel na kusababisha kifo cha Muisrali mmoja na kuwajeruhi wengine 2.Maafisa wa kijeshi wa Israel wamesema, mashambulio yake yalilenga majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wanamgambo kuweka silaha zao.Hapo awali,wanachama 4 wa kundi la Kipalestina la “Islamic Jihad” waliuawa katika mashambulio yaliyofanywa na ndege za Israel.Kwa upande mwingine,waziri wa miundombinu wa Israel,Binyamin Ben-Eliezer amesema,Israel iwalenge viongozi wote wa makundi ya wanamgambo.Vikosi vya ulinzi vya Israel,visitofautishe kati ya wale wanaofanya mashambulizi na wale wanaotoa amri aliongezea waziri Ben-Eliezer.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com