GAZA : Hamas yasema serikali mpya kutoitambuwa Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 14.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA : Hamas yasema serikali mpya kutoitambuwa Israel

Kundi la Kiislam la Hamas linaloongoza serikali ya Palestina limesema leo hii serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina inayopangwa kuundwa haitoitambuwa Israel au kukubali ufumbuzi wa mzozo wa Mashariki ya Kati kwa kuwepo mataifa mawili la Palestina na lile la Kiyahudi.

Msimamo huo utavuruga juhudi za Palestina kutaka kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi vya mataifa ya magharibi vya miezi minane kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itakuwa inakubalika zaidi kwa Israel na mshirika wake wa karibu Marekani.

Marekani na washirika wake katika kundi la pande nne la wasuluhishi wa mzozo wa Mashariki ya Kati wamewela vikwazo hivyo kuishinikiza Hamas ambayo iliuchukuwa madaraka ya Mamlaka ya Palestina hapo mwezi wa Machi kutambuwa haki ya kuwepo kwa taifa la Israel,kukanusha matumizi ya nguvu na kukubali mikataba ya amani ilioko hivi sasa.

Msemaji wa Hamas Fawzi Barhoum amesema wanakata ufumbuzi wa mzozo huo kwa kuwepo kwa mataifa mawili ambayo ni dira ya Rais George W Bush wa Marekani kwa sababu inawakilisha kutambuliwa moja kwa moja kwa Israel.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com