GAZA CITY:Majeshi ya Israel yaondoka Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY:Majeshi ya Israel yaondoka Gaza

Majeshi ya Israel yameondoka kwenye Ukanda wa Gaza jana usiku badaa ya operesheni iliyosababisha vifo vya wapiganaji 11 wa Palestina.Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Israel uvamizi wa roketi uliotokea katika eneo la Kati la Gaza na kaskazini umekwisha na majeshi kurudi.

Wapiganaji 6 kati ya 11 waliouawa ni wa kitengo cha wapiganaji cha kundi la Hamas lililoteka eneo la Gaza mwezi jana.

Zaidi wa Wapalestina 25 walijeruhiwa katika shambulio hilo kwa mujibu wa duru za hospitali.Wanajeshi wawili wa Israel pia walijeruhiwa katika operesheni hiyo ya Gaza iliyowahusisha wanajeshi 100 waliojihami kwa vifaru na helikopta.

Israel kwa upande mwengine inajitolea kuimarisha serikali mpya ya Rais wa Palestina Mahmoud Abbas japo kushikilia kuwa itanedelea kushambulia wanamgambo.Rais Mamhoud Abbas na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert wanatarajiwa kufanya mazungumzo mwezi huu mjini Jericho katika eneo la Ukingo wa Magharibi.Mazungumzo hayo yalikwama baada ya Hamas kuteka eneo la Ukanda wa Gaza.

Maafisa wa serikali wa Israel na Palestina walianza majadiliano kuhusu usalama mwanzoni mwa wiki hii ambayo Israel inataka yaendelee mara kwa mara katika miji ya Ramallah na Jerusalem .Majadiliano hayo yanalenga kufanikisha juhudi za kuunda jeshi la kitaifa usalama la Palestina.

Kwa upande mwengine Umoja wa Ulaya unataraji kwamba washiriki wa mazungumzo ya pande nne ambao ni Umoja wa Ulaya,Umoja wa Mataifa ,Marekani na Urusi watakutana katikati ya mwezi huu na wapatanishi wa mataifa ya Arabuni Misri,Jordan ,Saudia na Arabuni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com