GAZA CITY : Ukanda wa Gaza katika wasi wasi | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Ukanda wa Gaza katika wasi wasi

Ukanda wa Gaza uko kwenye hali ya wasi wasi leo wakati Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akiwa tena kwenye malumbano na chama tawala cha Hamas kuhusiana na vikosi vya kundi hilo la Kiislam.

Wapalestina watatu wameuwawa hapo jana katika mji wa Gaza katika mapambano kati ya makundi ya Hamas na lile la Fatah la Rais Abbas licha ya kufikiwa kwa makubaliano ya hapo Ijumaa kati ya Abbas na Waziri Mkuu Ismail Haniyeh wa kundi la Hamas ya kusitisha umwagaji damu kati ya makundi yao ambao umeuwa watu 13 na kujeruhi wengine zaidi ya 60 wiki iliopita.

Masaa machache kabla Rais Abbas alitaka Hamas ivunje kundi la wanajeshi wake wa wizara ya mambo ya ndani kikosi kinachojulikana kama kikosi kikuu kwa kusema kwamba kikosi hicho sio halali na kinapaswa kujumuishwa kwenye muundo wa jeshi la usalama uliopo hivi sasa.

Abbas pia ameamuwa kufanya mabadiliko kwenye vikosi vya usalama na uongozi wake.

Hamas imeushambulia wito huo wa Abbas kuwa ni kosa na kuonya dhidi ya hatua zozote zile kwa wanajeshi wake 5,500 na imesema kwamba itaongeza kikosi hicho maradufu.

Hamas imeonya hatua yoyote ile dhidi ya kikosi chake hicho itakabiliwa na hatua ya matumizi ya nguvu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com