GAZA CITY : Serikali mpya kutoitambuwa Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Serikali mpya kutoitambuwa Israel

Mshauri wa Waziri Mkuu wa Palestina wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh amesema serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Palestina haitoitambuwa Israel.

Ahmed Yousef amekaririwa akisema wakati serikali hiyo mpya itaheshimu mikataba ya amani iliopita na Israel haitojifunga kukubali haki ya kuwepo kwa taifa la Israel.

Hilo ni mojawapo ya sharti kuu lilioainishwa na kundi la pande linaloshughulikia amani ya Mashariki ya Kati kwa ajili ya kuondolewa vikwazo dhidi ya serikali inayoongozwa na Hamas. Makundi hasimu ya Hamas na Fatah yamesaini makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika mji mtakatifu wa Mecca nchini Saudi Arabia hapo Alhamisi.

Takriban watu 100 wameuwawa katika mapambano kati ya makundi hayo mawili tokea mwezi wa Desemba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com