GAZA CITY : Ndege za Israel zashambulia jengo la Hamas | Habari za Ulimwengu | DW | 17.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Ndege za Israel zashambulia jengo la Hamas

Ndege za kivita za Israel zimeshambulia kwa mabomu makao makuu ya Kikosi Kikuu cha kundi la Hamas katika mji wa Gaza leo hii.

Mtu mmoja ameuwawa na wengine 30 kujeruhiwa katika shambulio hilo.Mripuko huo wa mabomu umetibuwa ukimya wa wastani wakati wa asubuhi huko Gaza kufuatia siku kadhaa za mapigano makali kati ya makundi Hasimu ya Hamas na Fatah.

Takriban watu 20 wameuwawa wakati mapambano kati ya makundi hasimu ya Kipalestina ya Hamas na Fatah yakiendelea katika Ukanda wa Gaza.

Israel imesema itachukuwa hatua kali dhidi ya wanamgambo wa Kipalestina huko Gaza ambao wamevurumisha maroketi kadhaa katika miji ya Israel ilioko karibu katika siku za hivi karibuni.

Rais Mahmoud Abbas wa kundi la Fatah amefuta ziara yake iliopangwa kufanyika Gaza kwa ajili ya mazungumzo na Waziri Mkuu Ismael Haniyeh wa kundi la Hamas kujaribu kuinusuru serikali ya umoja wa kitaifa ambayo imeundwa na makundi hayo miezi miwili iliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com