1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY: Mashambulio ya Israel yameua Wapalestina 6

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD31

Shambulio lililofanywa na Israel kutoka angani kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabalya huko Gaza, limeua Wapalestina 6 na kuwajeruhi 18 wengine, raia wengi wakiwa miongoni mwao.Polisi wa Kipalestina wamesema tangu siku ya Alkhamisi, Wapalestina 20 wameuawa katika mashambulio ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.Azma ya mashambulio hayo ni kukomesha makombora ya kienyeji yanayorushwa kutoka eneo hilo hadi kusini mwa Israel.Tangu uasi wa Wapalestina kuzuka Septemba mwaka 2000,hadi watu 5.434 wameuawa,wengi wao wakiwa Wapalestina.