GAZA CITY : Mapigano ya Wapalestina yapamba moto | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Mapigano ya Wapalestina yapamba moto

Wapalestina wengine saba wameuwawa hapo jana katika mapambano kati ya makundi hasimu mjini Gaza na kufanya idadi ya vifo kutokana na mapambano makali ya siku tatu kufikia watu 22 na kuvuruga mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Miongoni mwa waliopoteza maisha yao ni mtoto wa miaka miwili na kijana wa miaka 16.Makundi hayo ya Fatah ya Rais Mahmoud Abbas na Hamas linaloongoza serikali ya Palestina yamefuta kufanyika kwa mazungumzo zaidi ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na kupamba moto kwa umwagaji damu.

Mapigano hayo yameanza Alhamisi usiku wakati wanamgambo wasiojulikana waliposhambulia gari la kikosi cha wizara ya mambo ya ndani kinachoongozwa na Hamas katika mji wa Jabalia kaskazini mwa ukanda wa Gaza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com